Saturday, 6 December 2014

WANADAMU

Tawaona wanadamu,wengi kiasi cha haja
kila mmoja na zamu,watakupiga pambaja
uunapovuja damu,watachoka kukutaja
na tatusiwa kwa hamu,hadi uvukedaraja
wanadamu ni viumbe,ni viumbe vya ajabu

Tawaona kila siku,maonzi kwako wewe
takudurusu ja buku,hata kipaa ja mwewe
kote utasakwa huku,hawatakuacha uwe
utachinjwa kama kuku,na mwishowe uliwe
wanadamu ni viumbe,ni viumbe vya ajabu

Tawaona nakwambia,hata unaposinzia
waatakunyemelea,na kamwe kukuvamia
hawatakuhurumia,waatakuparamia
hadi unapoumia,zaidi utaumia
wanadamu ni viumbe,ni viumbe vya ajabu

Tawaona kwa mwangaza,gizani ndani wamo
atakayekudekeza,yuko ndani ya shimo
milele unachoweza,takupatia ya mdomo
kiasi tumbo kujaza,ja kiongozi jomo
wanadamu ni viumbe,niviumbe vya ajabu

Tawaona daiima,wasichoke kuzunguka
ndiposa mimi Ndiema,natulia kwa miaka
na kamwe kutenda mema,hadi nipite mipaka
hatua lazima,nimeona kitendeka
wanadamu ni viumbe,ni viumbe vya ajabu

No comments:

Post a Comment