Sunday, 7 December 2014

DUNIA

Kamwe daima dawamu,mambo nimeyaona
nashindwa taisha zamu,angalau kuwe kona
juu naogopa damu,natumai nitapona
nimekubali mie,ina mambo dunia

Inazungumziwa ebola,nayo kote inauwa
wengi waja wanalala,utafikiri kalewa
maadamu tuko jela,lini tutafunguliwa
nimekubali mie,ina mambo dunia

ukimwi sijagusia,watu pia wanaugua
insi kote twaumia,mwishowe shindwa pumua
kaski ikitimia,mola milango fungua
nimekubali mie,ina mambo dunia

vita kote twapigana,kamwe hakuna huruma
amani sisi twanena,huku tumebeba chuma
lini waja watapona,tuwache kupanga njama
nimekubali mie,ina mambo dunia

No comments:

Post a Comment