Sikiza yote sikiza,lakini bagua mbaya
kilichoo nzuri tuza,huku ukifurahiya
wabaya nao fukuza,upeo hiyo... fikiya
mwishowe we!tabasamu,maono kitimiia
Tulia aah! tulia,wewe unda mikakati
tafuta njia fikia,vile hakuna wakati
usije ukajutia,nawe huyo pite kati
mwishowe we! tabasamu,maono kitimiia
Chakura wewe chakura,hadi yotee upate
maadui baki fura,mwagike chozi na mate
hata kama ni kwa kura, endaa wasikupate
mwishowe we!tabasamu,maono kitimiia
Pambana eeh! pambana,hadi jasho imwagike
ja kuku tafuta dona,mpaka ukingo ufike
na ile mbayaa kana,hadi mbarika pasuke
mwishowe we!tabasamu,maono kitimiia
Kimbia mkiki kimbia,wote uwaache nyuma
sala Mola husikia,afurahiie mama
majaliwa kitimia,ushindwe kamwe kupima
mwishowe we! tabasamu,maono kitimiia
No comments:
Post a Comment