Saturday, 6 December 2014

MVUA

Raha mie naona,tangu wewe nikuone
yote kabisa navuna,menidekeza ninone
tuvuke njia pana,kila mwia nikuone
kama kote inanyea,mapenzi itufurike

Kama penzi kikohozi,kwangu wewe dawa
meipata kwako dozi,kaponaa niko sawa
meifanya iwe kozi,kazi mekuwa kipawa
kama kote inanyea,mapenzi itufurike

Nishike mkono milele,kamwe niwe nawe
hata kuwe na kelele,kipusa yote upewe
tugange sote ya mbele,siku za usoni tuwe
kama kote inanyea,mapenzi itufurike

Wacha mi nikupapase,kidosho nikudekeze
wengine wasikuguse,mpira wetu tuucheze
upweke usitutese,raha sisi itujaze
kama kote inanyea,mapenzi itufurike

Malkia mependeka,wacha nikuchumbie
wakati wako mefika,mahaba nikupatie
sasa moto umewaka ,maji isiufikie
kama kote inanyea,mapenzi itufurike
 

1 comment:

  1. kweli kote inanyea mapenzi imefurika. love the poem.

    ReplyDelete