Maisha iliyo raha,yaliyoko nyumbani
huzifanya tabia silaha,kwako na duniani
tamati yake karaha,kufaidikako kaburini
samaki mkunje,angali mbichi
Adhabu isiyo rungu,hadhiraye kizimbani
salazo ni kwake mungu,jaji askutie ndani
simanzi lililo wingu,hukukithiri usoni
samaki mkunje,angali mbichi
Miaka zipunguwapo,na mvi kuja kichwani
maisha ngumu chaguwapo,majonzi tele usoni
ungalifu usemapo,tamatiyo maishani
samaki mkunje,angali mbichi
Bei haina wema,haifunzwi shuleni
haipewi naye mama,siri imo akilini
huanzia kwa heshima,isiyo na kifani
samaki mkunje,angali mbichi
No comments:
Post a Comment