Saturday, 6 December 2014

KUMBUKUMBU

Nakumbuka yote mimi,nilivyokupa mapenzi
kafunga kabisa ndimi,ukanisukuma ja nzi
roho kaipiga ngumi,lo!kumbe mi mwanafunzi
kumbukumbu aushini,zafanya tuwe makini

Mimi yote nilikupa,kanitesa niumie
we!uliona mifupa,nikose maana mie
usikose nilikopa,ninunue uvalie
kumbukumbu aushini,zafanya tuwe makini

Mwanzoni kanisikiza,ulinipa yako busu
wewe ukanipumbaza,nikawa wako mabusu
kumbe nilikuchukiza,kanitafutia kisu
kumbukumbu aushini,zafanya tuwe makini

Mtima umeidunga,jeraha mi nauguza
navuja nimeifunga,mimi naona tu giza
mzito roho ja mzinga,dunia umenifunza
kumbukumbu aushini,zafanya tuwe makini

Nani mimi nimpende,katafuta ngo! sioni
kazunguka kama mende,nachungulia vioni
tapata mi peremende?,angalau nimweke makaoni?
kumbukumbu aushini,zafanya tuwe makini

No comments:

Post a Comment